News

May 8th, 2012
Application Form
April 16th, 2012
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yasherehekea miaka 50 ya Uhuru
April 12th, 2012
Mhe. Prof. Anna Tibaijuka (Mgeni rasmi ) katika sherehe hizo

Extra Menu

Mradi wa kutambua miliki kwenye maeneo yaliyojengwa kiholela

Mradi wa kutambua miliki kwenye maeneo yaliyojengwa kiholela 

1.UTANGULIZI

Utekelezaji wa Mradi wa Kutambua Miliki Kwenye Maeneo Yaliyojengwa Kiholela ulianza mwaka 2004. Awamu ya pili ilianza 2007 na inaendelea. Mradi huu ni jitihada ya serikali ya kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa
kutumia ardhi.
2. KUKUA KWA MIJI KI HOLELA
  • Kasi ya ukuaji wa miji kufikia asilimia 8 kwa mwaka na kupanuka kwa mipakaya miji.
  • Uhaba wa viwanja vilivyopimwana vyenye huduma
  • Uhaba wa rasilimali watu, fedha na vifaa katika Halmashauri
  • Usimamizi hafifu wa mipango ya uendelezaji miji
  • Uvunjaji wa Sheria na Taratibu za Mipango Miji kwa wananchi walio wengi.
3. CHIMBUKO LA MRADI
               • Utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Ardhi ya mwaka 1995 inayotamka kuwa
                 makazi holela “hayatabomolewa isipokuwa yale yaliyojengwa kwenye maeneo hatari, bali yataboreshwa kwakuwekewa huduma za msingi kupitia mipango shirikishi”.
  • Sheria ya Ardhi ya mwaka1999 (Na. 4 ya 1999) kifungu cha 23 kinabainisha masharti ya Leseni ya Makazi katika maeneo yaliyojengwakiholela.
  • Utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi ya mw a k a 2 0 0 0 i n a y o l e n g a kuwawezesha wananchi kiuchumi kwa kuingiza sekta isiyo rasmi kwenye sekta rasmi kufufua mitaji mfu kuwa hai.Dar es Salaam inakadiriwa kuwa nanyumba zipatazo 500,000 ambazo kati ya hizo 400,000 sawa na asilimia 80 ziko katika maeneo yaliyojengwakiholela na hazitambuliwi kisheria
4. MALENGO YA MRADI
  • Kutambua miliki kwenye maeneo yaliyojengwa kiholela na kuandaa daftari la wamiliki.
  • Kuongeza usalama wa miliki kwa kutoa Leseni za Makazi zinazoweza kutumika kama dhamana ya mkopo na kupunguza maskini
  • Kudhibiti ukuaji wa maeneo yaliyojengwa kiholela na kuzuia uharibifu wa mazingira.
  • Kuunda mfumo thabiti wa kumbukumbu(database) wa kusimamia na kuratibu maendeleo ya ardhi katika maeneo yaliyojengwa kiholela na kuzuia uharibifu wa mazingira.
  • Kuboresha utoaji wa huduma kwa wananchi.
 
5. MANUFAA YA MRADI
  • Leseni ya Makazi inaongeza usalama wa miliki na kumwezesha mmiliki kutumia ardhi katika mfumo wa uchumi rasmi ili kupunguza umaskini.
  • Kupanua wigo wa mapato ya Serikali kuu na Manispaa kupitia kodi ya ardhi, majengo na ada nyingine hivyo kuboresha utoaji wa huduma za msingi kwa wananchi.
  • Mfumo wa kumbukumbu umeongeza ufanisi katika kutoa huduma kwa wananchi ikiwa ni pamoja na kuandaa Leseni za Makazi, na kuhamisha miliki.
  • Manispaa zimeongeza uwezo wa kusimamia na kudhibiti maendeleo ya ardhi katika maeneo yaliyojengwa kiholela
  • Kuzuia uharibifu wa mazingira unaofanywa na wananchi wanaojenga katika maeneo ambayo ni hatari.
  • Mtaa kuwa na Daftari la wamiliki kumeongeza usalama wa raia na mali zao.
  • Kutoa fursa kwa ajili ya kurasimisha maeneo haya kwa kuweka huduma za kiuchumi na kijamii kupitia mipango shirikishi, hatimaye kupata Hati kamili ya Kumiliki ardhi.