News
MKUTANO WA RCMRD WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
- Login to post comments
Printer-friendly version
Send to friend
PDF version
MKUTANO WA RCMRD WAFANYIKA JIJINI DAR ES SALAAM
Mkutano wa Nchi 18 wananchama wa Upimaji na Ramani wa Raslimali kwa Maendeleo (RCMRD) umefunguliwa jana (17/11/2011) na Katibu Mkuu wa Wizara ya Ardhi , Nyumba na Maendeleo ya Makazi, Bw. Patrick Rutabanzibwa jijini Dar es salaam. Mkutana huo ulihusisha Makatibu Wakuu wa wizara zinazohusika na ardhi wa nchi hizo na wataalamu wa upimaji na ramani ikiwa ni baada ya kikao cha maandalizi cha wataalam hao mapema wiki hii.
Pichani kulia ni Mwenyekiti wa mkutano Dr. S. D. Mqayunga na kushoto ni Mkurugenzi Mkuu RCMRD Dr, Hussein O Farah(Picha na Anna Massao). Picha iliyoko chini inaonesha baadhi ya Wajumbe wa nchi wakisikiliza meza kuu.
(Picha na Anna Massao)
Lengo kubwa la mkutano huu ni kusaidia nchi za Afrika katika masuala ya upimaji na ramani kwa ajili ya maendeleo. Mkutano huu ni wa 45 kufanyika baada ya ule wa Capetown, South Afrika. Makao makuu ya RCRMD yako jijini Nairobi na Tanzania ni miongoni mwa waanzilishi wa kituo hiki mwaka 1975. Hadi sasa RCRMD Inajumuisha nchi kumi na nane zikiwemo Tanzania, Kenya, Uganda, Sudan, Ethiopia, Botswana ,Namibia ,Zambia, Mauritius, Seychelles , Somalia, Comoros , South Africa, Rwanda, Burundi , Lesotho ,Malawi na Swaziland.
Mwenyekiti wa kikao hicho ambaye pia ni Mkurugenzi wa Upimaji na Ramani katika Wizara ya ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi Bw. Silas Mayunga anasema, ‘tunafarijika kupata fursa ya kuaandaa mkutano huu, maazimio yatasaidia katika kuimarisha shughuli za upimaji ardhi, utunzaji wa mazingira na mafunzo kwa wataalamu na pia nchi yetu imejitangaza.
Bwana Mayunga aliongeza kuwa Tanzania ni nchi ya kwanza barani Afrika kukamilisha mpango wa alama ya upimaji ardhi inayojulikana kitaalamu ‘geodetic network’ambazo ni 740 na kuweza kusimikwa nchi nzima na kuongeza kuwa 6 kati ya alama hizo zimepimwa kitaalamu kwa njia ya satelaiti na pia serikali ina mpango wa miaka mitano wa upimaji ardhi nchini na katika kutekeleza mpango huo serikali imekubali kuanzisha kituo cha kupokea picha za satelaiti kitakachojengwa mjini Dodoma.