News

May 8th, 2012
Application Form
April 16th, 2012
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi yasherehekea miaka 50 ya Uhuru
April 12th, 2012
Mhe. Prof. Anna Tibaijuka (Mgeni rasmi ) katika sherehe hizo

Extra Menu

Wizara ya Ardhi yaibwaga Kahama Mining Ltd

Submitted by alexkaraba on Wed, 11/23/2011 - 11:27
Wizara ya Ardhi yaibwaga Kahama Mining Ltd
Na Anna Massao.
Wizara ya Ardhi yaibwaga Kahama Mining Ltd
 
Na Anna Massao.
Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi imeshinda kesi yake dhidi ya kampuni ya uwekezaji ya kigeni ya Kahama Mining Corporation  Ltd. kuhusu eneo la kiwanja kilichopo eneo la Oysterbay.
Hayo yalisemwa jana na Prof. Anna Tibaijuka, Waziri wa Ardhi, Nyumba na Makazi katika mkutano wake na waandishi wa habari ambapo ulifanyika ukumbi wa habari Maelezo jijini Dar- es- Salaam.  waziri huyo pia aliongozana na Katibu Mkuu wa wizara hiyo Patrick Rutabanzibwa, Mkurugenzi wa Mipango miji, kamishna wa Ardhi na Mwanasheria wa wizara hiyo.
 
Prof. Tibaijuka aliongeza kuwa baada ya uamuzi wa mahakama kuitaka wizara yake kurudisha kiwanja ambacho kwa sasa kimejengwa shule ya Sekondari ya Bongoyo waliamua kukata rufaa ambapo walishinda kesi hiyo, akizungumzia suala hilo pia Katibu Mkuu Patrick Rutabanzibwa alisema, ‘’ Tunaishukuru mahakama ya rufaa kwasababu imetenda haki kwa manufaa ya Watanzania”
Chanzo cha mgogoro huo ni baada ya kampuni hiyo ya kigeni kumilikishwa ardhi na Halmashauri ya wilaya Kinondoni ikishirikiana na Oysterbay Properties  Ltd.  bila kuishirikisha wizara husika  ambayo baadae ilitoa kibali cha kujengwa kwa shule hiyo ya sekondari na kampuni hiyo kuamua   kuishtaki baada ya kukataa eneo lingine la wazi walilopewa.
 
Profesa pia aliongoza zoezi la kuweka mabango eneo la Sinza ili kuonesha wananchi kuwa maeneo hayo ni ya wazi na hayastahili kuuzwa wala kujengwa na kuwataka wananchi wanaoishi kwenye maeneo ya wazi kuhama katika maeneo hayo.